Home » Robert Mbui:Jopo La Uteuzi Wa IEBC Limeegemea Kenyq Kwanza

Robert Mbui:Jopo La Uteuzi Wa IEBC Limeegemea Kenyq Kwanza

Mbunge wa Kathiani Robert Mbui amedai kuwa jopo la uteuzi la kuajiri Mwenyekiti na wanachama wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) lilibuniwa ili kuunga mkono muungano wa Kanya Kwanza.

 

Mbui, akizungumza kwenyeruninga moja humu nchini leo hii Jumanne, ameteta kuwa jopo la uteuzi halina usawa kwa vile muungano wa Azimio la Umoja one-kenya haukupewa nafasi ya kutoa uanachama wake wakati jopo hilo lilipobuniwa.

 

Mbunge huyo anadai kuwa haiwezekani kukiacha chama kikuu cha kisiasa kama Azimio kuwakilishwa katika mchakato huo.

 

Kulingana na Mbunge huyo Azimio inadai kuundwa upya kwa jopo hilo ili kuruhusu uwakilishi wa haki katika bodi ya uchaguzi.

 

Jopo hilo la wanachama 7 likiongozwa na Nelson Makanda liliteuliwa mwezi Februari na Rais William Ruto jambo ambalo lilifungua zoezi la kuajiri makamishna wapya.

 

Aidha Jopo hilo lilihitajika kuwa na wawakilishi wa Tume ya Utumishi wa Umma (PSC), Kamati ya Uhusiano ya Vyama vya Kisiasa (PPLC), Chama cha Wanasheria wa Kenya (LSK), na Baraza la Dini Mbalimbali la Kenya.

 

PSC na Baraza la Dini Mbalimbali la Kenya zilitengewa wanachama wawili (mwanamume na mwanamke) kila moja huku PSC, PPLC na LSK zikiwa na mwanachama mmoja aliyependekezwa kwenye jopo.

 

Kwa upande wa mbunge wa Belgut Nelson Koech ambaye ni wa mrengo wa kenya kwanza amedai rais William ruto hangeruhusu wanasiasa kuendesha zoezi hilo la kuwapiga msasa wanaotaka kujaza nafasi hiyo kwani watawapendelea watu wanaowafahamu ili kujiimarisha kisiasa.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!