Home » Mwanamume Anayeshukiwa Kumnajisi Bintiye Wa Miaka 2 Akamatwa Kirinyaga

Mwanamume Anayeshukiwa Kumnajisi Bintiye Wa Miaka 2 Akamatwa Kirinyaga

Polisi kutoka kituo cha polisi cha Wanguru eneo la Mwea Mashariki kaunti ya Kirinyaga wamemkamata mwanamume anayeshukiwa kumnajisi msichana wake wa miaka miwili na nusu.
Inasemekana kwamba mtoto huyo aliachwa na mamake ambaye alitofautiana na mumewe wakati kisa hicho kilipotokea.

 

Wakaazi wa kijiji cha Kiumbu waliitikia kilio cha mtoto huyo, lakini mwanamume huyo alifanikiwa kutoroka Muda mfupi baadaye, alinaswa na wakaazi waliogadhabishwa ambao walikuwa wakimtafuta.

 

Akithibitisha kisa hicho OCPD wa Mwea Mashariki James Mutua amesema kuwa polisi walitokea baada ya kupokea taarifa kutoka kwa wananchi.

 

 

Mutua amesema mtoto huyo wa miaka miwili na nusu alikuwa akitibiwa katika Hospitali ya Kaunti ndogo ya Kimbimbi ambapo ripoti ya matibabu ilifichua kuwa alikuwa amenajisiwa.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!