Home » Moto Umeteketeza Nyumba Za Polisi Nyandarua

Maafisa wa Polisi huko Olkalou, Kaunti ya Nyandarua wameanzisha uchunguzi kubaini chanzo cha moto ulioteketeza nyumba tano za polisi katika kituo cha polisi cha Gichungo usiku wa Jumapili.

 

Moto huo unaripotiwa kuanza saa 1.00 usiku ukiteketeza vitu kadhaa vikiwemo baiskeli na pikipiki zilizokuwa zimezuiliwa na maafisa hao wa polisi.

 

Aidha Hakuna aliyejeruhiwa wakati wa kisa hicho, ambacho kulingana na mzee wa eneo hilo Githinji Mwaniki kisa hicho kimeacha eneo hilo katika hali hatari ya usalama.

 

Mwaniki ametoa wito wa kuingilia kati haraka kusaidia kujenga nyumba mpya kwa vile kituo cha polisi kinahudumia eneo kubwa la Olkalou.

 

Ikumbukwe kwamba kituo hicho cha polisi kilijengwa kupitia uhamasishaji wa jamii kufuatia kuongezeka kwa visa vya wizi katika maeneo ya Gichungo na Kariamu.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!