Home » Seneta Methu Akosolewa Na Wakenya

Seneta wa Nyandarua John Methu amekashifiwa na wakenya baada ya kudai utumizi wa picha ya kiongozi wa upinzani Raila Odinga kwenye chupa za pombe ili kukabiliana na ulevi katika eneo la mlima Kenya.

 

Katika chapisho kwenye Twitter seneta huyo alisema kujiepusha na hali hiyo kunaweza kuwa suluhu katika vita dhidi ya tishio la ulevi katika eneo la Kati, ambapo kiwango cha unywaji pombe haramu ni asilimia 4.1 karibu maradufu ya kitaifa.

 

Methu, hata hivyo, alipendekeza kuwa hii inaweza tu kuafikiwa ikiwa chupa za pombe zitatiwa chapa ya picha za kiongozi wa muungano wa Azimio la umoja one-Kenya Raila Odinga .

 

Seneta huyo ambaye pia ni mwananchama wa chama cha (UDA) anadai kuwa hii itawafanya wakazi wengi kuacha kunywa pombe moja kwa moja kutokana na kile alichokitaja kuwa wakazi wengi wa mlima kenya wanachukizwa na kiongozi huyo wa upinzani.

 

Maoni ya Methu yanajiri wiki moja tu baada ya Naibu Rais Rgathi Gachagua kuitisha mkutano wa viongozi wakuu wa mlima Kenya mjini Nyeri mnamo Ijumaa, Aprili 14, kujadili suala la ulevi na utumizi wa dawa za kulevya katika eneo hilo.

 

Gachagua alisema Rais William Ruto alimwagiza kuandaa mkutano huo uliohudhuriwa pia na Waziri wa Mambo ya Ndani Kithure Kindiki akiwaleta pamoja viongozi wa kitaifa, wale wa kaunti, waliochaguliwa na utawala kutoka kaunti tano za iliyokuwa Mkoa wa Kati… kati yao Kiambu, Murang’a, Nyeri, Nyandarua na Kirinyaga kuja na mapendekezo ya kukabiliana na pombe haramu na matumizi mabaya ya dawa za kulevya.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!