Home » Viongozi Wa Bonde La Ufa Wamsuta IG Koome Kuhusu Matamshi Ya Barua Ya Raila ICC Badala Ya Kukabiliana Na Ujambazi Eneo Hilo

Viongozi Wa Bonde La Ufa Wamsuta IG Koome Kuhusu Matamshi Ya Barua Ya Raila ICC Badala Ya Kukabiliana Na Ujambazi Eneo Hilo

Viongozi wa Bonde la Ufa wamemsuta Inspekta Mkuu wa Polisi Japhet Koome kwa kushindwa kukabiliana na majambazi eneo hilo.

 

Viongozi hao ambao walikuwa walikutana kwa maombi ya madhehebu mbalimbali katika eneo la Sirate huko Baringo walimkashifu Koome kwa kuangazia majibizano na Kiongozi wa Azimio Raila Odinga na kwa kiasi kikubwa kutokuwa na uwezo wa kukabiliana na majambazi.

 

Kulingana na viongozi hao wamemtaka Inspekta Jenerali aonyeshe azma aliyokuwa nayo kudhibiti visa vya uhalifu nchini kuwabana majambazi bonde la ufa.

 

Katika wiki iliyopita, majambazi hao walikuwa wameua watu wawili na kujeruhi kadhaa na kuiba ng’ombe 70 huko Baringo Kusini.

 

Katika tukio lingine lililokejeli idara ya polisi ni majambazi waliwahadaa maafisa wa usalama kumpeleka kamanda wao hospitalini.

 

Kamanda wa majambazi hao alikuwa amepigwa risasi huko Baringo na maafisa wa polisi walidanganywa kwamba alikuwa mwathiriwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Iten katika Kaunti jirani ya Elgeyo Marakwet.

 

Yakijiri hayo….katibu mkuu wa UDA cleophas Malala amedai kuwa chama cha ODM kinachoongozwa na Raila Odinga kinawakandamiza wakenya wanaochipuka kisiasa kwa kupendelea jamii moja ya Luo kufaidika na nyadhifa za uongozi serikalini.

 

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!