Home » Professor Jay Arejea Tena Hadharani

 

Mwanamuziki nguli nchini Tanzania katika miondoka ya HIP HOP Joseph Haule ambaye anajulikana kama Proffesor Jay amerejea tena baada ya kuwa kimya kwa zaidi ya takribani siku 460 alipotangazwa kuugua.

 

SOMA PIA:Rayvanny Amshusha Diamond Platnumz YouTube

 

Siku ya Jumanne jioni, Jay alirejea kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo  aliutumia kuandika kwa urefu zaidi kwa kutoa shukrani kwa watu wote ambao walifanikisha suala lake la kuuguzwa mpaka kurejea katika hali aliyonayo.

 

 

Katika waraka huo Jay aliwashukuru watu mbalimbali akiwemo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe, vituo vya habari kama vile Clouds FM, Wasafi FM, pamoja na Millard Ayo kwa mchango wao wa dhati juu ya michango na afya yake.

 

Mwanamuziki huyo ambaye pia alikuwa mbunge wa Mikumi alimshukuru mke wake kipenzi, familia yake pamoja na Mwenyezi Mungu kwa kurejea tena katika afya yake.

 

Kwa zaidi ya mwaka mmoja, uliopita ilitolewa taarifa ya kuwa anasumbuliwa na maradhi ya Ini ambayo yalimfanya awe kimya kwa muda.

 

Professor ni mmoja kati ya wanamuziki wenye historia kubwa nchini Tanzania katika upande wa muziki katika kazi zake kama vile albumu yake ya Machozi, Jasho na damu pamoja na Mapinduzi halisi.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!