Mwanaume Australia Aweka Rekodi Ya Kupiga Push-ups
Mwanaune mmoja kutoka Australia ameweka rekodi mpya ya dunia ya kupiga push-ups, akikamilisha zaidi ya 3,206 kwa saa moja tu hiyo ni 53 kila dakika, au karibu moja kwa sekunde.
Lucas Helmke alipiga push-ups kwenye gym yake huko Brisbane na kutwaa taji lililowekwa na mwanamume mwingine wa Australia mwaka jana tu ni mara ya nne kwa rekodi mpya kuwekwa kwa mafanikio katika miaka mitatu.
Mhasibu wa biashara, mwenye umri wa miaka 33 aliiambia Guinness World Records alitaka “kutoa msukumo” kwa mtoto wake wa mwaka mmoja kwa kumwonyesha “hakuna lisilowezekana.”
Kila push up ilibidi isiwe na dosari ili kufikia viwango vinavyohitajika kwa rekodi rasmi ya dunia.
Helmke alitakiwa kuuweka sawa mwili wake akielekea juu, bila kukunja magoti na kiuno chake, huku akifikia angalau pembe ya digrii 90 kwenye kiwiko cha mkono alipojishusha.
Alipandishwa kizimbani mara 34 kwa sababu ya umbo lisilofaa, na bado aliendelea kuwapita waweka rekodi waliokuja mbele yake.
Rekodi ya hapo awali iliwekwa na Daniel Scali, ambaye alipiga push-ups 3,182, mnamo Aprili 2022.
Helmke alivunja rekodi hiyo kwenye ukumbi wa Iron Underground Gym Novemba mwaka jana na hivi majuzi alifahamishwa na Guinness World Records kwamba rekodi yake imeidhinishwa.
Akichapisha cheti hicho kwenye Facebook mwezi uliopita, aliandika: “Hatimaye hiki kilifanikiwa.”
Helmke aliiambia Guiness World Records ilimchukua miaka miwili hadi mitatu kujiongezea nguvu ili kuweza kufanya kazi hiyo isiyo ya kawaida.
Kutokana na ushindani huo, haijafahamika rekodi yake itasimama kwa muda gani.
Vyombo vya habari vya eneo la Florida mnamo Machi viliripoti kwamba mwanamume Mmarekani Rob Stirling, 60, aliweza kupiga push-ups 3,264 mwishoni mwa mwezi uliopita – lakini madai hayo bado hayajatambuliwa na Guiness.
Helmke wakati uo huo tayari ana vituko vyake kwenye rekodi zingine.