Home » Tedd Josiah Asema Sautisol Itasahaulika Hivi Karibuni

Tedd Josiah Asema Sautisol Itasahaulika Hivi Karibuni

Mtayarishaji wa muziki nchini Kenya Tedd Josiah ameeleza mawazo yake kuhusu muziki wa Kenya na kutoshirikishwa kwa serikali katika kuhifadhi utamaduni wa muziki.

 

Tedd Josiah alisema kuwa bendi ya Sautisol ya Kenya wanafanya vizuri kwa sasa lakini baada ya miaka 20 watakuwa wamesahaulika.

 

“Vijana wanafanya vizuri kwa sasa, lakini nikuhakikishie ndani ya miaka 20 hakuna mtu atakayezungumza juu yao. Watakuwa wamesahaulika kabisa. Unajua kwanini, kwa sababu kama nchi hatufanyi kazi ya kutosha kuhifadhi utamaduni wetu wa muziki na urithi.”

 

Tedd alisema kuwa katika mataifa mengine, serikali inajihusisha na utunzaji wa muziki ili kuhakikisha hata vizazi vijavyo vinawafahamu wasanii wakubwa waliowahi kuitawala tasnia ya muziki huo.

 

“Nchi nyingine utakutana na vituo vya utamaduni vinavyosimulia historia ya muziki wao, hatumzungumzii Fundi Konde na Daudi Kabaka wote hawa walikuwa wasanii wakubwa lakini hakuna cha kuonyesha safari yao hakuna anayetuongelea. sasa. Ndivyo itakavyotokea kwa Sauti Sol siku zijazo.”

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!