Home » Sifuna Afichua Siri Ya Azimio

Seneta wa Nairobi, Edwin Sifuna amezungumzia jinsi kiongozi wa Azimio Raila Odinga alipanga kuwadhibiti Naibu Rais Rigathi Gachagua na viongozi wengine wenye misimamo mikali ndani ya Kenya Kwanza wanaodaiwa kupinga mazungumzo ya amani.

 

Akihojiwa na runinga moja humu nchini, seneta huyo wa awamu ya kwanza amefichua kuwa Raila aliagiza timu ya watu 14 iliyochaguliwa na Azimio La Umoja One-kenya kuiwakilisha katika vyama viwili kuacha kujihusisha na vita vya maneno na makabiliano ya hadharani na vigogo wa rais Ruto.

 

Sifuna amedokeza kuwa, kama Azimio, hawakuzingatia matamshi yaliyotolewa na Gachagua, mwanauchumi David Ndii, na Kiongozi wa wengi katika Bunge la Kitaifa Kimani Ichung’wah kuhusu mapatano ya Raila na Ruto.

 

Mnamo Alhamisi, Aprili 6, Gachagua alisema kwamba ikiwa Rais angepeana mkono na Raila, atajitenga na mchakato wa mazungumzo.

 

Sifuna amesema kuwa ingawa Azimio utaendelea kupuuza matamshi hayo, watarejea kwa maandamano ikiwa mazungumzo yao hayataafikiwa.

 

Wanachama hao ni; Seneta Ledama Ole Kina wa (Narok), Seneta Edwin Sifuna wa (Nairobi), Seneta Enock Wambua wa (Kitui),wabunge Millie Odhiambo wa (Suba Kaskazini), Amina Mnyazi wa (Malindi), David Pkosing wa (Pokot Kusini) na Otiende Amollo (Rarieda)

 

Kenya Kwanza intarajiwa kutaja timu yao ya wabunge kushiriki katika mazungumzo ya pande mbili leo hii Jumanne.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!