Home » David Ndii Asema Serikali Ya Ruto Inaweza Kukata Tamaa

David Ndii, Mwenyekiti wa Baraza la Washauri wa Kiuchumi la Rais William Ruto amesikitishwa alipokuwa akiwajibu wakosoaji waliodai serikali imeshindwa kuwalipa wafanyikazi wake mishahara.

 

Ndii kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, alimjibu mtaalamu wa masuala ya mawasiliano aliyeshauri serikali ya Rais William Ruto kuanza kwa kufungia malipo na marupurupu yote kwa wale walio juu ikiwa imeshindwa kulipa mishahara.

 

Hapo awali, alipokuwa akizungumza kwenye runinga moja humu nchini, alijitetea dhidi ya madai kuwa alikuwa anatetea serikali ilihali kwa sasa mi wazi kuwa kuna mwanya mzito, akidai kuwa alikuwa mkweli na kuchora taswira halisi ya uchumi.

 

Akielezea hali hiyo, Ndii amebainisha kuwa ubadhirifu huo katika vyombo mbalimbali vya serikali ulifanywa kimakusudi na serikali iliyopita.

 

Kulingana na Ndii, serikali inafaa kuweka mifumo itakayokomesha ufujaji wa fedha za umma kimakusudi, ikiwemo kuimarisha afisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

 

Kuhusu suala la madeni, Ndii amepuuzilia mbali ripoti kuwa serikali haikufilisika wakati wa utawala uliopita na kushikilia kuwa utawala wa Rais Ruto umeweza kulipa madeni ambayo yalikuwa yakisubiri.

 

Hata hivyo, Ndii amewahakikishia watumishi wa umma kuwa serikali inajaribu kujaza pengo hilo kwa kukopa kutoka soko la ndani ambapo inakumbana na changamoto mbalimbali na kusababisha kucheleweshwa kwa mishahara ya wafanyikazi wa umma.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!