Dalai Lama Aomba Msamaha Kwa Kumtaka Kijana Aunyonye Ulimi Wake
Kiongozi wa kiroho wa Tibet ameomba msamaha kwa umma na kwa kijana ambaye alimwomba pambaja na muumini huyo kumtaka amnyonye ulimi.
Kwenye video inayodaiwa kurekodiwa mwezi Februali, 28 nchini India katika Hekalu la kiongozi huyo Dharamshala, kijana mdogo anaonekana kwenye video akiomba kukumbatiwa na kiongozi huyo kimyume na matarajio, anamwuuliza iwapo yuaweza kumnyonya ulimi.
Dalai anautoa ulimi wake nje kutaka kunyonywa ila kijana yule mdogo anasonga nyuma ishara ya mshtuko.
Akidhania yameisha, Dalai anamsogeshea kijana yule kipaji chake apigwe busu ila pia anaonekana kukaidi huku waumini wakiangua kicheko na wengine kushangilia.
Kwenye mtandao wa Twitter, afisi ya Dalai Lama imepachapisha ujumbe wa kumwomba kijana yule msamaha pamoja na familia yake na marafiki kwa maneno ya maudhi ambayo kiongozi huyu aliyasema na yaweza kumkosesha kijana yule na umma kwa ujumla amani, na pia kupungua kwa sifa.
“Kiongozi huyu hupenda utani na kutangamana na watu. Wakati mwingi hunaswa kwenye kanda akifanya utani na hata kando ya kamera akisema anonywe ulimi” afisi yake Dalai ilisema kwenye ujumbe.
Nchini Tibet, kunyonywa ulimi kulianzishwa na Mfalme Lang Darma aliyetambulika kwa ulimi wake mweusi Karne ya Kumi na Tisa kama njia ya salamu na kuanzia hapo, waumini nchini Tibet husalimiana kwa njia ya kunyonywa ulimi.
Aidha, kwa kuwapo kwa uvamizi wa Wachina nchini humo- Tibet, Dalai Lama alitorokea nchini India mwaka 1959 kama mkimbizi na ameishi kule na kufanya makazi.
Dalai mwenye umri wa miaka 87, mwaka 2022 kwenye mahojiano na shirika la BBC, alinaswa akisema kwamba yeyote atakayeurithi utawala wake hasa wa jinsia ya kike, awe mwanamke mwenye sura nzuri na ya kuvutia.
Maneno yake yalizua mtafaruku na kejeli kutoka himaya ya waumini wa Tibet na umma kwa ujumla duniani waliompinga kwa maneno yake ya ubaguzi hadi kuomba msamaha.