Home » Serikali Ya Kaunti Ya Migori Kugharamia Matibabu, Mazishi Ya Waathiriwa Wa Ajali Ya Lori

Serikali Ya Kaunti Ya Migori Kugharamia Matibabu, Mazishi Ya Waathiriwa Wa Ajali Ya Lori

Serikali ya Kaunti ya Migori italipa bili za matibabu kwa watu saba waliojeruhiwa na gharama za mazishi ya watu wanane waliofariki kwenye ajali Jumamosi asubuhi.

 

Haya yanajiri baada ya lori lililokuwa likisafirisha mchele hadi mji wa mpakani wa Isebania, kupata hitilafu ya breki na kuanguka katika mji wa Migori.

 

Gavana wa Migori Ochilo Ayacko, kwenye kikao na wanahabari kilichofuata, alisema timu itaundwa kuhakikisha kuwa waliojeruhiwa wanapata matibabu yote yanayohitajika kisha kutoa ripoti kuhusu gharama ili serikali ya kaunti hiyo iweze kusuluhisha shughuli hiyo.

 

Gavana Ayacko pia alisema kuwa serikali yake itashirikiana kwa karibu na polisi kubaini chanzo cha ajali hiyo na pia kuweka vipimo ili kuepusha ajali kama hizo katika siku zijazo.

 

Kamanda wa polisi kaunti ya Migori Mark Wanjala alithibitisha kuwa watu wanane walifariki na watu saba kujeruhiwa katika ajali hiyo iliyotokea baada ya lori aina ya tipper kupata hitilafu katika mji wa Migori na kuwagonga watumiaji wengine wa barabara.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!