Home » Gari La Polisi Latumbukia Mtoni Kirinyaga, Wanne Wajeruhiwa

Watu wanne wakiwemo maafisa wawili wa polisi walijeruhiwa baada ya gari la polisi kutumbukia kwenye mto Rupingazi kaunti ya Kirinyaga Jumapili asubuhi.

 

Gari la Polisi wa Utawala (AP) lilitumbukia kwenye mto ulio karibu na barabara kuu ya Mwea -Embu.

 

Kulingana na kamanda wa polisi wa Mwea -East Daniel Kitavi, gari hilo lilikuwa likielekea kituo cha mafunzo cha AP cha Kanyonyo Kitui kutoka Nyeri.

 

Kitavi alisema dereva wa gari la polisi alikuwa akijaribu kukwepa kumgonga mwendesha bodaboda ambaye alipata tatizo la pikipiki kando ya daraja la Rupingazi.

 

Kitavi alisema maafisa wa polisi wa trafiki kutoka kituo cha polisi cha Wang’uru walifika mara moja na maafisa hao na waendesha bodaboda walikimbizwa katika hospitali ya Embu Level Five baada ya kupata majeraha.

 

Mwakilishi wa Wadi ya Njukiini, Timothy Kariuki alisema alishtuka kwani ajali ilitokea baada tu ya kuvuka daraja la Rupingazi.

 

Kitavi alisema maafisa wa polisi wanajaribu kuliondoa gari hilo mtoni na wamelinda silaha za waathiriwa.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!