Home » Rosa Ree Amwaga Machozi, I’m Not Fine

 

Mwanamuziki wa Hip Hop kwa upande wa wanawake nchini Tanzania Rosa Ree asubuhi ya Tarehe 8 Aprili aliianza kwa kuueleza hisia zake kwa mashabiki mara baada ya kuchapisha video yake katika mtandao wake wa Instagram na kueleza ya kuwa hayuko sawa.

 

SOMA PIA:Mange Ashauri Basata

 

Mwanadada huyo ambaye amekuwa akitamba na kibao chake cha Blue Print pamoja na Albumu yake ya GODDESS alichapisha video hiyo huku ikimuonesha akiwa analia kwa uchungu na kuendelea kusema ya kuwa “I’M NOT FINE”

 

 

Pamoja na video hiyo lakini pia mwanadada huyo pia aliambatanisha maneno aliyoyaandika yakiwa yanasema ya kuwa

 

IM NOT FINE! Mara nyingi naulizwa “How are you?” Nasema “I’m fine” kusema tu ila sio kumaanisha. But now I admit IM NOT FINE!……..

 

Baada ya chapisho hilo kusamba katika mitandao ya kijamii, wasanii wenzake pamoja na mashabiki hawakuweza kumuacha nyuma kwa kuzidi kumtia moyo ya kuwa hiyo ni hali ya kawaida katika maisha. Baadhi ya wasanii hao ni pamoja na muigizaji Rose Ndauka, Gigy Money pamoja na Mimi Mars.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!