Home » Mashabiki Wa Zuchu Wafurahishwa Na Tuzo Za Tanzania

 

Mashabiki wa mwanadada anayetamba kwa sasa na kibao cha  Napambana Zuchu, wamefurahishwa na Baraza la Sanaa la Taifa BASATA mara baada ya msanii wao huyo kupata nafasi ya kuwania vipengele sita katika Tuzo za Tanzania Music Awards.

 

SOMA PIA:Zuchu Apewe Heshima Yake

 

Zuchu ambaye Kwa mwaka jana hakufanikiwa kushiriki tuzo hizo kutokana na uongozi wa lebo yake ya WCB Wasafi kutokupendekeza majina ya wasanii wao, amefurahisha mashabiki zake kwa mwaka huu kupata nafasi katika tuzo hizo.

 

 

Katika tuzo za TMA Zuhura aliwekwa katika vipengele vitano ikiwemo Mtumbuizaji bora wa mwaka wanawake, Mwanamuziki Bora wa kike, Mwanamuziki Bora wa kike Bongo Fleva, Video Bora ya mwaka pamoja na Wimbo Bora wa mwaka Bongo Fleva

 

Licha ya hayo yote kwa Sasa bado mjadala ni kuhusu mapungufu yaliyoko katika tuzo hizo huku wasanii kama Baraka de Prince, Mbosso pamoja na Rayvanny wakimwaga mapovu juu ya tuzo hizo kuwajawa na upendeleo.

 

Lakini pia Basata kupitia kwa mratibu wa tuzo hizo, Mzee Mrisho aliyefanya mahojiano na Rick Media kwa njia ya simu aliwataka wasanii watulize jazba na kuelezea ya kuwa endapo kuna msanii yeyote ambaye atahitaji ufafanuzi basi anakaribishwa katika makao makuu ya Ofisi za Barasa kwa ajili ya ufafanuzi zaidi.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!