Home » IG Koome Awaonya Madereva

Inspekta Jenerali wa Polisi Japhet Koome amewahakikishia Wakenya usalama wao wakati wa likizo ya Pasaka wanapokusanyika katika maeneo tofauti ya taifa kwa sherehe.

 

Katika taarifa leo hii Alhamisi, Koome amebainisha kuwa ufuatiliaji na kuweka hatua zinazofaa ili kuhakikisha usalama unaimarishwa.

 

Ameongeza kuwa maafisa watatumwa vya kutosha kwa barabara kuu, maduka makubwa, viwanja vya ndege, vituo vya reli na mabasi, mahali pa ibada, na vituo vya burudani.

 

Mkuu huyo wa polisi, hata hivyo amesema kuwa takwimu zimeonyesha kuwa idadi kubwa ya ajali za barabarani hurekodiwa wakati wa likizo ambayo imesalia kuwa sababu kuu ya majeraha na vifo.

 

Hivyo amewataka madereva wote wa magari kuwa waangalifu wanapotumia barabara na kuzingatia sheria za trafiki zilizowekwa.

 

Pia ametahadharisha kuwa baadhi ya barabara zinaweza kujaa maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na madereva wa magari wanapaswa kuwa waangalifu.

 

Koome pia ametoa onyo kwa madereva wazembe ambao watakuwa wakiendesha gari wakiwa wamekunywa vileo, akisisitiza kwamba watakamatwa.

 

Sherehe za Pasaka huanza Ijumaa, Aprili 07 na kumalizika Jumatatu, Aprili 10.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!