Home » Kagame: Nikistaafu Nitakuwa Mwandishi Wa Habari

Kagame: Nikistaafu Nitakuwa Mwandishi Wa Habari

Rais wa Rwanda Paul Kagame amekiri anapania  kustaafu na kukabidhi madaraka baada ya miaka 23 uongozini.

 

 

Akizungumza katika kikao na wanahabari pamoja na rais wa Kenya Dkt William Samoei Ruto Kigali, Rais Paul Kagame amefichua mikakati ya urithi wake unajadiliwa kikamilifu na chama tawala, cha RPF.

 

 

Kagame ametaja  kustaafu kwake kuwa hatua isiyoepukika.

 

 

Bw. Kagame alisema si lazima kuwa na nia ya kuchagua mrithi wake bali ni kuweka mazingira yatakayoleta watu wanaoweza kuongoza.

 

 

 

 

Hata hivyo Kagame hataelekea  nyumbani akisaafu bali atabadilisha taaluma tu.

 

 

“Nina uhakika siku moja naweza kujiunga na uandishi wa habari katika uzee wangu. Ninatazamia hilo,” Bw Kagame alisema.

 

 

Maoni yake yanakuja siku chache baada ya chama tawala nchini humo, Rwandan Patriotic Front (RPF-Inkotanyi), kumchagua mwanamke wa kwanza kuwa makamu mwenyekiti.

 

Kagame atasalia kuwa mwenyekiti, nafasi ambayo ameshikilia tangu 1998 na alichukua usukani wa uongozi wa taifa hilo mwaka wa 2000.

Uchaguzi mkuu wa Rwanda utafanyika Agosti 2024 na Kagame anataraijiwa kuwania tena.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!