Home » Raila: Sina Haja Ya Kusalimiana Na Gachagua

Kiongozi wa  Azimio Raila odinga ameweka wazi kuwa iwapo upande wa Kenya Kwanza hautaonyesha nia yoyote katika mazungumzo ambayo wamekubaliana na rais William ruto, basi hatakuwa na lingine ila kuendelea na maadamano.

 

 

‘’Tumesema na bado tunarudia kuwa hatutaki handsheki, wale wa Kenya Kwanza ndio wanaitisha.Kusema ukweli, sina haja ya kusalimiana na Gachagua’’

 

Amesema mambo waliokuwa wakiangazia wakati wa maandamano lazima yashughulikiwe vikamilifu bila  kufeli.

 

Baadhi ya mambo ambayo Azimio inapendekeza ni kushushwa kwa gharama ya maisha, kufunguliwa kwa sava ya IEBC na kurejeshwa kwa makamishana wote wa IEBC walioshurutishwa kujiuzulu.

 

 

Aidha, Odinga sasa anaitaka serikali kugharamia matibabu ya hospitali ya wale wote waliojeruhiwa wakati wa maandamano wiki iliyopita. Amelaani unyama uliotekelezwa na polisi wakati wa maandamano.

 

 

Vile vile, Odinga amependekeza kuundwa kwa tume kama ilivyokuwa wakati wa Kofi Annan Mwaka wa 2008 ambapo jopo kutoka ndani na nje ya bunge ili kushughulikia mambo yaliyoangaziwa.

 

 

Azimio pia imesema tayari wako na majina ya watu watakao jumuishwa kwa tume hiyo wakati wake ukifikia

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!