Home » Rais Ruto Kuondoka Nchini Kwa Ziara Ya Siku Mbili Nchini Rwanda

Rais Ruto Kuondoka Nchini Kwa Ziara Ya Siku Mbili Nchini Rwanda

Rais William Ruto ataondoka nchini leo kwa ziara ya Kiserikali ya siku mbili katika taifa la Rwanda.

 

Kwa mwaliko wa mwenyeji wake Rais Paul Kagame, Wakuu hao wa Nchi mbili wanatarajiwa kujadiliana kuhusu maeneo yenye maslahi na ushirikiano, ikiwa ni pamoja na miradi ya ushirikiano wa Ukanda wa Kaskazini, usalama wa chakula, uvumbuzi, afya na elimu.

 

Ziara hiyo pia inatarajiwa kuimarisha ushirikiano wa kibiashara ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Bara la Afrika, huku viongozi hao wawili wakisisitiza tena dhamira yao ya mtangamano wa EAC na ushirikiano wa eneo la Biashara Huria la Bara la Afrika (A.C.F.T.A) kwa ajili ya ukuaji wa uchumi.

 

Amani na usalama wa kikanda pia ni baadhi ya masuala muhimu yatakayojadiliwa itakayofikia kilele cha kutiwa saini kwa mikataba baina ya nchi hizo mbili.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!