Home » Rais Ruto Aanzisha Mchakato Wa Kushughulikia Masuala Yaliyoibuliwa Na Raila

Rais Ruto Aanzisha Mchakato Wa Kushughulikia Masuala Yaliyoibuliwa Na Raila

Rais William Ruto ameanza mchakato wa kuangazia masuala yaliyoibuliwa na upinzani kuhusiana na makamshna wapya wa tume ya uchaguzi na mipaka IEBC miongoni mwa mengine .

 

Kwa makataa ya wiki moja kutoka kwa Odinga, Rais Ruto alikutana na viongozi wa Bunge la Kitaifa na Seneti kutoka upande wa wengi ambapo aliwataka kutanguliza uundaji wa jopokazi kutoka pande mbili.

 

Kiongozi wa wengi katika Bunge la Kitaifa Kimani Ichung’wa anasema wako tayari kufanya jinsi Rais Ruto atakavyowaelekeza.

 

Ichung’wa ameongeza kuwa wameafikiana juu ya muundo ambao jopokazi la pande mbili litapitisha na kuonyesha kuwa huenda ikawa kamati ya muda ambayo muundo wake utaamuliwa na wabunge kwa kushauriana na viongozi wa chama.

 

Ikumbukwe kwamba hatua ya Rais Ruto ya kuunda jopokazi jipya la kuwateua makamshina wapya wa IEBC inaacha jopo lililobuniwa awali katika hali ya sintofahamu.

 

Jopo hilo lilikuwa limetangaza wiki jana kukamilika kwa orodha ndefu ya waliotuma maombi ya uenyekiti na makamishna ambapo Wakenya 25 waliomba kuchukua nafasi ya Wafula Chebukati kama Mwenyekiti wa IEBC huku wengine mia 895 wakitazamia nafasi sita za makamishna zilizoachwa wazi.

 

Huenda jopo hilo likalazimika kusitisha zoezi la uajiri ili kupisha mchakato huo wa pande mbili.

 

Huku Wakenya wakisherehekea utulivu uliotokana na maandamano yaliyositishwa, Macho yote sasa yanaelekezwa kwenye bunge na lini mchakato wa kuunda kamati ya mashauri ya pande mbili utaanza,…? nani watakuwa wanachama na ikiwa mwisho, mchakato huo utakuwa mzuri.

 

Leo hii rais ruto amefungua rasmi hafla ya kongamano kuu la ulinzi wa kijamii jijini Nairobi.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!