Home » Wanafunzi Miongoni Mwa Abiria Waliohusika Katika Ajali Baringo

Wanafunzi Miongoni Mwa Abiria Waliohusika Katika Ajali Baringo

Kundi la wanafunzi kutoka shule ya upili ya Ngetmoi Girls, na mwalimu wao, leo walihusika katika ajali ya barabarani karibu na barabara kuu ya Tenges-Kabarnet, huko Baringo ya Kati.

 

Mkuu wa shule hiyo Joyce Namasaka amethibitisha kisa hicho.

 

Wanafunzi hao saba walikuwa kwenye gari aina ya Nissan Shuttle – pamoja na abiria wengine ajali hiyo ilipotokea mita kadhaa kutoka shuleni.

 

Habari zinasema kuwa wanafunzi hao wamepata majeraha mabaya, na kulazimika kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Baringo pamoja na abiria wengine.

 

Kwa sasa wasichana watatu wapo katika hali nzuri, huku wawili wakilazwa hospitalini.

 

Kulingana na Vincent Kibet aliyeshuhudia kisa hicho, gari hilo lilitoka nje ya barabara lilipokuwa likiongeza kasi na kubingiria mara kadhaa.
Mwalimu aliyekuwa pamoja na wanafunzi hao alikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Eldoret akiwa amepata majeraha mabaya.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!