Home » Mbunge wa Molo: Rais Ruto, Raila Wanapaswa Kuhakikisha IEBC Wana Uwezo

Mbunge wa Molo: Rais Ruto, Raila Wanapaswa Kuhakikisha IEBC Wana Uwezo

Mbunge wa Molo Kuria Kimani ametoa wito kwa Rais William Ruto na kinara wa upinzani Raila Odinga kuhakikisha kwamba watu watakaoteuliwa katika Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) wana uwezo.

 

Akizungumzia mtazamo wa pande mbili uliochukuliwa na Ruto na Raila, Kimani amesema iwapo wawili hao wanalenga kuunda upya IEBC ili kutimiza maslahi yao ya kisiasa, wanapaswa kuachana na hatua hiyo.

 

Akiongea katika shule ya upili ya Arimi iliyoko Molo, mbunge huyo amemsifu Rais kwa kuchukua uamuzi huo wa kuwahusisha viongozi wa Azimio, akisema kuwa lengo hilo litahimiza amani na utulivu nchini.

 

Baada ya kutoa wito kwa upinzani kusitisha maandamano yake, Rais William Ruto alikutana na uongozi wa wengi katika Seneti na Bunge la Kitaifa jana Jumatatu ili kuanza mchakato wa kuzingatia masuala yaliyoibuliwa na upinzani, ikiwa ni pamoja na kuunda upya IEBC.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!