Home » Mchungaji Dorcas Rigathi Kuunda Vikundi Vya Wajane Kuwawezesha Kujimudu

Mchungaji Dorcas Rigathi Kuunda Vikundi Vya Wajane Kuwawezesha Kujimudu

Mke wa Naibu Rais Mchungaji Dorcas Rigathi anasema amejitolea kuunda vikundi vya kitaifa ya wajane ambavyo vitasaidia wanawake kupata fedha za kuendeleza maisha yao.

 

Akizungumza katika eneo la Loitoktok Kajiado alipokutana na vikundi vya wajane chini ya (Osigili Nkoliaei) kutoka Kajiado Kusini Mchungaji Dorcas amesema ofisi yake itashughulikia maslahi yao na kufadhili shughuli za kuwawezesha wajane.

 

Chini ya ufadhili wake anasema vikundi hivyo vitakuwa na wawakilishi kutoka kaunti 47 kote nchini ili kuwasaidia kuunda vyama vya ushirika ambavyo sio tu vitawasaidia kumiliki mashamba bali pia kumiliki nyumba.

 

Pia Mchungaji Dorcas amewataka wanawake hao kumsaidia kufanikisha ajenda yake ya kuokoa mtoto wa kiume kwa kuisaidia serikali katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya katika maeneo yao kwa kuwang’oa wanaofanya biashara ya dawa za kulevya.

 

 

Ameelezea wasiwasi wake juu ya kuongezeka kwa idadi ya wavulana mitaani na kuongeza kuwa ofisi yake inafanyia kazi mpango wa ukarabati wa wavulana hao.

 

Mchungaji Dorcas amesema kuwezeshwa kwa mtoto wa kiume kutasaidia pia katika mapambano dhidi ya ukeketaji katika maeneo ya nchi. Kwa kudai kuwa jamii itasaidia katika kubadili fikra za wanaume (Wavulana) kuheshimu wanawake na kuelewa mwanamke aliyepata ukeketaji si bora zaidi.

 

Kamishna wa Kaunti ya Kajiado Felix Watakila alisema baadhi ya maeneo ya kaunti bado yanakumbana na ukeketaji.

 

Kuhusu LGBTQ Mchungaji Dorcas amesisitiza msimamo wake akisema kwamba nchi haitasukumwa na tamaduni za kimagharibi na kupindua tamaduni, sheria na imani zake.

 

Hafla hiyo pia imehudhuriwa na Mbunge wa Kajiado Kusini Parashina Sakimba na Kamishna wa Kaunti ya Kajiado Felix Watakila miongoni mwa viongozi wengine.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!