Home » Jamaa Wa Boda Boda Ashtakiwa Kwa Mauaji Ya Mbunge Nairobi

Jamaa Wa Boda Boda Ashtakiwa Kwa Mauaji Ya Mbunge Nairobi

Mwendesha bodaboda Philip Mweteli amefunguliwa mashtaka ya kumuua Mbunge wa Banisa Kullow Maalim Hassan.

 

Mweteli ambaye alifika mbele ya Hakimu Mkuu Mwandamizi wa Milimani Esther Kimilu mnamo Ijumaa, Machi 31 alikana kumpiga Kullow katika eneo la South B jijini Nairobi.

 

Pia alikanusha mashtaka mengine ya kushindwa kuripoti ajali hiyo kwa polisi na kuendesha pikipiki bila leseni.

 

Mshtakiwa aliachiliwa kwa dhamana ya Ksh 300,000 pesa taslimu na bondi mbadala ya Ksh 500,000.

 

Kullow alifariki Jumatano, Machi 29 katika Hospitali ya Aga Khan alikokuwa akipokea matibabu baada ya kugongwa na pikipiki kando ya Barabara ya Mombasa.

 

Habari za kifo chake zilisambazwa kwa mara ya kwanza na mwenzake katika Bunge la Kitaifa Adan Keynan, Mbunge wa Eldas.

 

Kullow aliingia bunge mara ya kwanza mwaka wa 2017 na alikuwa anatumikia muhula wake wa pili

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!