Amber Ray Na Jimal Wafuatiliana Kwenye Mitandao

Amber Ray na aliyekuwa mpenzi wake mfanyabiashara Jimal Rohosafi wameonekena kufuatiliana saa chache tuu baada ya AMBER na Kenneth Rapudo kuachana. Wawili hao hawajawahi kuwa marafiki mtandaoni tangu walipoachana vibaya mnamo 2021.
Uchunguzi wa haraka kwenye mitandao yao ya kijamii unaonyesha kuwa wawili hao kwa sasa wanafuatilia kila mmoja kwenye Instagram. Amber ameachana na mpenzi wake Rapudo na kum-unfllow kwenye Instagram.
Amber pia amefuta picha zao za furaha wakiwa pamoja kwenye ukurasa wake wa Instagram. Katika tangazo lake leo, Amber alisema amechoka kuwa katika mapenzi. Aliandika:
“Siku mpya ya kuanza kama mama pekee wa watoto wawili. Done with love,” aliandika kwenye hadithi zake za Insta.
Kwa upande wake, Rapudo alisema uwongo ndio sababu ya wawili hao kuachana. Alisema:
“Uongo una tofauti nyingi sana. Ukweli hauna. Katika chini ya miezi miwili, sote tutajua ukweli na sababu ya kuachana. Ni hayo tu kwa sasa,” aliandika.
Rapudo alisema zaidi kwamba atamtunza mtoto wake ikiwa yeye na Amber wako pamoja au la.
Amber pia alituma onyo zito kwa wapenzi wake wa zamani ambao wanaanza kuchapisha mambo kumhusu mtandaoni baada ya kuachana.
Katika ujumbe wake wa hivi majuzi, Amber alionya kuwa atamjibu mwanaume yeyote anayepanga kumharibia jina baada ya kuachana nao.
“Kuna hii tabia ya watu wakitoka maishani mwangu wanakimbia sana mitandao ya kijamii na kuanza kunichafulia jina na nimekaa kimya na siri zao mpaka leo… ila nimechoka sasa. Iwapo yeyote kati ya marafiki au wapenzi wa ex wangu) atakuja kwa ajili yangu, we jua niko tayari kwenda kuzimu na kurudi! Wakati huu nitapigania myself’