Home » Raynanny Atumia 70M Kwa Video Yake Mpya

Rayvany apata upalozi CRDB

 

Mmiliki wa lebo ya Next Level Music na mwanamuziki Raymond Mwakusya almaarufu kama Rayvany amefunguka  kuwa ametumia kiasi cha shilingi milioni 70 kufanya video yake inayofuata.

 

Kupitia ukurasa wake wa Instastory, Vannyboy ameandika akielezea  kuwa gharama hizo amezitumia ili kuhakikisha ya kuwa mashabiki zake wanapata kitu kizuri.

 

NIMETUMIA SIKU SABA KUSHOOT MY NEXT VIDEO NA KILA SIKU SIYO CHINI YA 10M KUSHOOT. IT’S ALL ABOUT GOOD MUSIC AND NICE VIDEOS FOR MY FANS

 

Mashabiki wa Rayvany kwa sasa wako macho juu kungojea ngoma hiyo haswa kwa upande wa video ambayo mshindi huyu wa tuzo ya BET ameinadi kutumia gharama kubwa ya milioni 70 za kitanzania

 

SOMA PIA:CRDB Wamtangaza Rayvanny Kama Balozi Mpya

 

Mwezi mmoja uliopita ndio Vannyboy aliachia kazi yake ya mwisho aliyoipa jina la Senorita aliyomshirikisha mwanamziki na mwandishi Gims kutokea nchini Congo

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!