Home » Ubelgiji Kusaidia Kenya Kutengeneza Dawa za Saratani

Ubelgiji Kusaidia Kenya Kutengeneza Dawa za Saratani

Taifa la Ubelgiji imetangaza kuunga mkono ajenda ya maendeleo ya Kenya kupitia ushirikiano katika biashara na uwekezaji, afya na nishati mbadala.

 

 

Pia itaunga mkono mipango ya amani na usalama katika kanda na kukabiliana na hali ya hewa.

 

 

Rais William Ruto na Waziri Mkuu wa Ubelgiji Alexander De Croo walitia saini Mkataba wa Maelewano kuhusu Mashauriano ya Kisiasa ambao utatoa mfumo wa mashirikiano kuhusu mambo ya kibiashara.

 

 

Akizungumza katika Ofisi ya Waziri Mkuu mjini Brussels, Ubelgiji, Waziri Mkuu Croo alijitolea kuunga mkono ajenda ya usalama wa chakula nchini Kenya.

 

 

Kuhusu afya, Kenya itashirikiana na makampuni ya Ubelgiji ya Bioteknolojia kuanzisha kampuni za insulini, chanjo na kutengeneza dawa za saratani nchini.

 

 

Ubelgiji pia itaunga mkono azma ya Kenya kudumisha amani na utulivu kwa ajili ya ustawi wa eneo hilo.

 

 

Viongozi hao wawili walikubaliana kufanya kazi pamoja ili kuendeleza ukuaji wa sekta ya nishati mbadala nchini Kenya na kukuza usimamizi wa mikopo ya kaboni.

 

 

Maeneo mengine ya ushirikiano yaliyojadiliwa ni pamoja na usimamizi wa bandari, uchumi wa kidijitali na msimamo wa Kenya kuhusu vita vya Ukraine.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!