Usalama Waimarishwa Katika Shamba La Kenyatta Baada Ya Uporaji Mali
Zaidi ya saa 24 baada ya Shamba la Northlands linalomilikiwa na familia ya rais wa zamani Uhuru Kenyatta kuvamiwa na watu wasiojulikana, serikali sasa imetuma maafisa wa polisi wametumwa eneo hilo kupiga doria.
Maafisa hao waliwasili mwendo wa saa nne asubuhi kwa minajili ya kulinda mali inayomilikiwa na familia hiyo ya Kenyatta.
Hii ni baada ya mamia ya watu wasiojulikana mnamo Jumatatu kuvamia ardhi hiyo na kuharibu mali.
Kundi hilo lililokuwa na misumeno ya umeme na mapanga walikata miti kadhaa nakujigawia mashamba na wengine kuanza kujenga vibanda.
Baadaye walitoroka na idadi isiyojulikana ya kondoo. Ilipotimia jioni, kundi hilo la vijana liliwasha moto na kuharibu mali ya thamani isiyojulikana.
Hii ni baada ya wao kuvunja uzio na kuzunguka shamba hilo kubwa.
Walioshuhudia walisema genge hilo lilipata ardhi kutoka upande wa Kamakis yenye shughuli nyingi na wengine walionekana wakiwa wamebeba kondoo kutoka kwa mali hiyo.
Hadi kufikia sasa, hakuna taarifa yoyote imetolewa kutoka kwa serikali ama kwa kitengo cha usalama kuhusiana na uhuni huo na uporaji wa mali ya kibinafsi ya rais mwanzilisha wa taifa la kenya.
Tayari, Mamlaka Huru ya Uangalizi wa Polisi ilisema Jumatatu inachunguza ni kwa nini walishindwa kutoa ulinzi kwa shamba hilo