MC Jessy Afunguka Kuhusu Kutopata Kazi Ya CAS
Mcheshi MC Jessy alitambulishwa Alhamisi, Machi 23 kama balozi wa chapa ya pombe Glendale.
Akizungumza baada ya kutambulishwa, MC Jessy alisema kuwa anafurahia ushirikiano huu mpya.
Pia alifunguka kuhusu kutotajwa miongoni mwa walioteuliwa kwenye nyadhifa za CAS.
“Yes many people have called me hey Jessy hatujaona jina yako, well I can tell you I’ve been in the circle’s si ati nilikuwa nangoja jina yangu, personally kuna vitu tulikuwa tumeongea na President na hizo ni zetu personal.
“So I wasn’t waiting for CAS, I can for sure tell you, I didn’t apply coz I know vile tuliongea I know our chief hustler ni mtu wa ku fulfill promises.
“Akikuambia atakufanyia kitu ukweli kweli ye ni wa kusema na kutenda” Jessy told.
Alisema kuna mipango mingine.
“Popote atakaponihitaji nitakuwepo, ila najua tulichojadili faragha, coz si huona na si huongea.
I will wait for coz sina haraka, ndio maana unaniona tuko huku tunazindua bidhaa na kufanya brands coz tunajua vitu tulivyoongea”
“Unajua naweza sema nina mtu waseme umenikana, unaona? ni mgani alafu naweza sema sina mtu na anjulikana, so about relationships and all mi ni msee nakuanga mserious sana the reason why I dont talk much about my personal love life family life and all I have is that your personal life is the softest point of attack.
Any person who wants to attack you ata attack mahali roho yako iko so I like keeping it private like that so that people dont bother into hizo vitu ”
Alisisitiza kuwa atabaki faragha.
“Hata ukiendelea kuniuliza ninatoka na nani, sitakuambia kamwe kwa sababu huwa nadhani hakuna mtu anayetaka kujua, kwa sababu huwa nadhani ni hatua laini ya kushambulia adui anapotaka kukumaliza atakuja kwako. watoto watakuja kwa mke wako watakuja kwa mpenzi wako, kwa mchumba wako na mtu mwingine yeyote ambaye yuko katika maisha yako” alifichua kuhusu uamuzi wake.
Alisema anafurahi kuweka maisha yake hivyo licha ya tetesi zisizokwisha kuwa anatoka kimapenzi na Shix Kapienga.
“Unaona unapozungumzia watu wengine wakati hawapo unakuwa hautendei haki kwa sababu mnafaa mtuone nikiwa na yeye ndio tunamuuliza tukiwa wawili, lakini kumzungumzia mtu mwingine wakati hawapo, wakati mwingine huwa sijisikii ni vizuri sana. , unahitaji kuwa nayo”