Home » WHO Yaonya Ugonjwa Wa Kifua Kikuu Umeanza Kuenea Tena

WHO Yaonya Ugonjwa Wa Kifua Kikuu Umeanza Kuenea Tena

courtesy ozone

Kenya imejiunga na ulimwengu kuadhimisha siku ya ugonjwa wa kifua kuu ambapo wito umetolewa kwa wakenya kuwa waangalifu na kuajiadhari hususan msimu huu wa baridi.

 

Kinara wa Mawaziri Musalia Mudavadi ambaye aliongoza ujumbe wa serikali katika sherehe za leo katika uwanja wa Huruma county ya Uasin Gishu, amesema serikali imeweka mikakati yote ya kumaliza ugonjwa wa kifua kiku nchini.

 

Amesema mafunzo jinsi ya kujikinga na TB inaendelea kwa sasa kote nchini na kufichua madawa vile vile yamesambazwa ya kutosha katika hospitali za umma nchini.

 

Haya yanajiri wakati shirika la afya duniani, WHO, likisema Idadi ya vifo vya kifua kikuu hususan bara Ulaya imeongezeka tena ikilinganishwa na miongo miwili iliyopita.

 

Kulingana na utafiti uliyotolewa na WHO, TB imewaangamiza watu zaidi ya  27,300 barani uropa mwaka wa  2021 ikilinganishwa na 27,000 mwaka uliopita,.

 

WHO imesema ongezeko la Ugonjwa wa kifua kiku mwaka wa 2021 ulitokana mlipuko wa covid 19 ambayo huduma zote zilielekezwa kwa janga hilo na vile vile matumizi ya madawa zisizo na nguvu ya kutibu TB.

Shirika hilo limesema hii ndio ilikuwa mara ya kwanza kwa zaidi ya miaka 20 ya ungonjwa wa TB kuenea  kwa kasi mno

 

Urusi na Ukraine ndizo nchi mbili zilizoathiriwa zaidi, na karibu vifo 8,500 vimeripotiwa katika mataifa haya mawili.

 

Ugonjwa huo husababishwa na bakteria ambayo kimsingi hushambulia mapafu.

 

Inasambazwa kupitia hewa na watu walioambukizwa, kwa mfano kwa kukohoa. TB Inazuilika na inatibika.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!