DStv, GOtv Kupeperusha Mubashara Pigano La Mandonga Na Lukyamuzi
Pigano linalosubiriwa kwa hamu na ghamu dhidi ya Karim Mandonga na mganda Kenneth Lukyamuzi litapeperushwa moja kwa moja kuanzia saa moja usiku kutoka ukumbi wa Kasarani Gymnasium siku ya Jumamosi tarehe 25 mwezi huu.
Pambamo hilo litapatikana kwa watazamaji wote wa GOtv na DStv.
Akizungumza wakati wa upimwaji wa uzani katika makau makuu ya Multichoce, katibu mkuu wa chama cha ndondi nchini Julius Odhiambo mabodia wote wanaoshiriki pigano hilo kutoka Tanzania na Uganda wamewasili.
“Matayarisho yote yamekamilika kwa ajili ya pambano hilo litakalohusisha pigano saba. Tunafurahi kwamba GOtv na DStv zitapeperusha hafla hiyo moja kwa moja kwenye DStv na GOtv,” alisema Odhiambo.
Wakati wa hafla hiyo hiyo, mkurugenzi mkuu wa MultiChoice Kenya, Nancy Matimu alithibitisha kuingia rasmi kwa MultiChoice katika tasnia ya ndondi inayokua kwa kasi nchini ili kusaidia kuwaonyesha wachezaji ubora wa mchezo huu huku watazamaji wa DStv na GOtv wakiendelea kuburudika.
“MultiChoice Kenya imejitolea kustawisha maisha kupitia vipindi ambayo yanaelimisha na kufahamisha, pamoja na kuburudisha hasa wakati huu ambapo Wakenya wanakabiliwa na shinikizo kubwa la kiuchumi. Nia yetu katika vipindi ya humu nchini haiwezi kulinganishwa na hii ni mara ya kwanza tunawapa Wakenya burudani ya moja kwa moja ya ndondi za hapa nyumbani huku tukiwaweka wanariadha wetukatika anga za kimataifa ,” alisema Nancy.
Pambano hilo dhidi ya Kenneth Lukyamuzi wa Uganda litakuwa pambano la Mandonga la pili la Pro Boxing jijini Nairobi baada ya Mtanzania huyo kumshinda Mkenya Daniel Wanyonyi katika pambano lisilo la ubingwa.