Home » Epuka Kula Nyama Inayouzwa Katika Maduka Makubwa, Wakenya Waambiwa

Fresh chicken meat on supermarket shelf, all logos removed

Taasisi ya Utafiti wa Matibabu ya Kenya (KEMRI), kwa ushirikiano na Shirika la Kulinda Wanyama Ulimwenguni, Kituo cha Utafiti wa Mikrobiolojia, imewatahadharisha Wakenya kuhusu nyama ya nguruwe na kuku wanaouzwa katika maduka makubwa(supermarkets).

 

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na watafiti hao, nyama inayouzwa kwenye maduka hayo ilikuwa na viwango vya bakteria sugu ambao walikuwa na madhara kwa watumiaji.

 

Zaidi ya mwaka mmoja, sampuli zilikusanywa kutoka kwa maduka makubwa katika miji mitano, ambayo ni Nairobi, Kisumu, Nakuru, Nanyuki, na Eldoret, na majaribio yalifanywa katika taasisi ya serikali.

 

Kulingana na Victor Yamo, mwanasayansi anayeshughulikia Ulinzi wa Wanyama Ulimwenguni, shida huanzia shambani wakati mkulima anaweka nguruwe na kuku kwenye makazi machafu.

 

Alilinganisha hali hiyo na janga, ambapo maisha milioni tatu yalipotea na KUsema kuwa ikiwa hali hiyo itaendelea, angalau watu milioni 10 wanaweza kufa kila mwaka.

 

Mnamo 2019, mwanahabari Dennis Okari alifichua jinsi maafisa wa maduka makubwa wasio waaminifu wanavyotumia kemikali kuongeza muda wa matumizi ya bidhaa za nyama.

 

Katika onyesho hilo, mhudumu wa duka kubwa alieleza kwa kina jinsi kemikeli aina ya (salfa) inavyotumika kwenye nyama ili kuifanya ionekane mbichi na kupunguza hasara.

 

Hatua hiyo ya uchunguzi ilizua mjadala miongoni mwa Wakenya waliotaka serikali kuingilia kati.

 

Aliyekuwa Waziri wa Afya wakati huo, Sicily Kariuki, alihakikisha kwamba Wizara ilikusanya sampuli kutoka kwa maduka mbalimbali na ingeshiriki matokeo ya uchambuzi na umma.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!