Home » Catherine Masitsa Ajiunga na Kipindi Cha ‘The Real Housewives Of Nairobi’

Catherine Masitsa Ajiunga na Kipindi Cha ‘The Real Housewives Of Nairobi’

Showmax show ‘The real housewives of Nairobi imeongeza idadi mpya kwa waigizaji wake, Dkt. Catherine Masitsa, mwanzilishi na mkurugenzi mkuu wa Samantha’s Bridal ndiye wa hivi punde.

 

Dkt. Catherine Masitsa ambaye pia ni daktari wa mifugo, mwekezaji wa mali isiyohamishika na mchapishaji, atafanya maonyesho yake ya kwanza Alhamisi, Machi 23 kama mama wa nyumbani wa sita akiungana na wanawake wengine watano walioanzisha kitengo hicho: Susan Kaittany, Vera Sidika, Sonal Maherali, Minne Kariuki, na Lisa Christoffersen.

 

Catherine ameonyesha kufurahishwa kwake na kujiunga na onyesho hilo, na kusema kuwa itakuwa fursa nzuri kwa mashabiki wake kumfahamu zaidi.

 

“Nimefurahi sana kuwa sehemu ya show hii kwa sababu mimi sio mkubwa sana kwenye mitandao ya kijamii, na nadhani kupitia The Real Housewives of Nairobi, mashabiki wangu watapata kuniona halisi nikiishi maisha yangu ya ajabu.”

 

Licha ya kujiunga na onyesho hilo vipindi vinne baadaye, Masitsa alisema amefurahia majibizano yake na akina mama wengine wa nyumbani na anafurahishwa na jinsi kila kitu kilivyo kweli.

 

Hatua hii ya Mfululizo inafuatia wanawake mashuhuri na waliofanikiwa wanapopitia maisha yao ya kifahari, mahusiano na kazi zao huko Nairobi, Kenya. Kipindi hiki kinatiririka kwenye Showmax na vipindi vipya kila Alhamisi.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!