Home » Boutross Munene Azungumzia Picha Zake Za Kisiri Zilizovuja

Rapa kutoka nchini Kenya, Boutross Munene amezungumzia picha zake za siri zilizovuja ambazo zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii.

 

Akizungumza kwenye mahojiano na Ankali Ray, Boutross alisema aliye kwenye picha hizo ni yeye lakini mazingira yalikuwa tofauti.
Alisema kuwa picha hizo zilipigwa miaka 4 iliyopita na video vixen ambaye alichukua nafasi yake.

 

“Sina shida na picha kwa sababu sikufanya chochote kibaya nilikuwa mwanadamu tu na kuna mtu alichukua fursa hiyo.”

 

Boutross alisema mwanamke huyo alikuwa vixen katika moja ya video zake na alitumia picha hizo kupata dakika chache za umaarufu.

 

Aliongeza kuwa haoni sababu ya kumchukulia hatua za kisheria kwa kuwa hataweza kumlipa na pia anataka kuwa mfano mzuri kwa wale wanaomtegemea.

 

Rapa huyo alisema tatizo lake ni kwa mwanablogu Edgar Obare, kwa sababu anashare picha hizo bila hata kujaribu kumpigia ili kupata stori moja kwa moja na itaishia kumgharimu pesa na biashara.

 

Alifichua kuwa hatua zozote dhidi ya mwanablogu huyo zitaamuliwa na timu yake.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!