Home » Gachagua Awaambia Wakenya Kupuuza “Likizo” Ya Jumatatu

Naibu Rais Rigathi Gachagua amewataka Wakenya kupuuza shinikizo la kiongozi wa muungano wa Azimio la Umoja One-Kenya Raila Odinga kwamba Jumatatu ni siku ya mapumziko, akiwashauri badala yake wafanye biashara zao kama kawaida.

 

Gachagua amehakikishia jumuiya ya wafanyabiashara na wawekezaji kwamba vyombo vya usalama viko macho kukabiliana na vitendo vyovyote vya uvunjaji sheria ambavyo huenda vikatoka kwa waandamanaji wa kundi la upinzani siku hiyo.

 

Akizungumza mjini Nanyuki wakati wa Tuzo za Uandishi wa Habari za Bima ya Pan-African (Re), Gachagua ametaja maandamano na hatua ya Azimio kama wingu la kupita, akisisitiza kwamba serikali iko thabiti na ina udhibiti kamili.

 

Alimtaja kiongozi yeyote asiye na uzalendo ambaye anajaribu kuleta hofu kwa uchumi unaojitahidi kujiimarisha kwa kuwachochea Wakenya, akiongeza kuwa utawala wa Rais William Ruto umejitolea kuboresha maisha ya wananchi kwa kuwashawishi wawekezaji.

 

Haya yanajiri huku Odinga na viongozi wa muungano wa Azimio wakitangaza maandamano makubwa jijini Nairobi siku ya Jumatatu kupinga gharama ya juu ya maisha miongoni mwa masuala mengine.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!