Hatimaye Joh Makini Aidondosha Wave
Mwamba wa Kaskazini Joh Makini ameachia EP yake ya kwanza iliyopewa jina la Wave kwa maana ya wimbi ikiwa imebeba jumla ya midundo sita ya Hiphop.
SOMA PIA: Burna Boy Kutumbuiza Katika Fainali Ya Ligi Ya Mabingwa Ulaya
Hii ni EP ya kwanza kwa Joh ambayo pia ameshirikisha wasanii akiwemo Damian Sol aliyepita naye katika Too Much, G Nako katika mkwaju wa Nyeusi sambamba na Ottuck William katika kichupa cha Success.
Baada ya AIR WEUSI kuachiliwa kama kundi kutoka kwa Weusi mwaka 2021 sasa ni zamu ya Joh Makini kama msanii binafsi kufanya kazi yake mwenyewe na ya kujivunia nayo.
Kama moja ya hatua kubwa aliyoifanya Chalii ya R katika mchakato mzima ya uandaaji wa EP yake hii ya kwanza kwa mkongwe huyu wa HIPHOP unaweza kusema SUCCESS IS A HAPPINESS