Meja Kunta Awashirikisha Marioo, Mabantu katika Demu Wangu Remix
Mkali wa nyimbo za Singeli kutokea Tanzania Meja Kunta amekuja tena na Remix ya goma lake Demu Wangu Remix lililoteka masikio ya wapenzi wa burudani haswa wapenzi wa nyimbo za Singeli akiwashirikisha Marioo pamoja na kundi maarufu la Mabantu.
Ni masaa machache tu tangu mkali huyo aachie kipande cha video kikionesha akiwa anarekodi video na Marioo na baada ya muda wa masaa kadhaa kupita wimbo huo ukaachiliwa.
Kwa upande wake Marioo si mara ya kwanza kwa yeye kupita atika migundo ya Sindeli baada ya kufanya vizuri katika kibao cha Nakuja Remix alichooshirikishwa na Balaa Mc.
SOMA PIA: Abigail Chams Kuachia Video Ya Nani
Kwa upande wao Mabantu wameua katika wimbo huu ambao kwa pamoja wameeleza juu ya maahusiano yanayotaka kubomoka baada ya mwanamke kupata mpenzi mwingine lakini kwa mapenzi pamoja na gharama zilizotumika vijana wanagoma kuvunja huba hilo.
Upande wa Video ukali umeangukia katika utashi wa Director Folex mnyama aliyefanya video kali kama vile Napambana kutoka kwa Zuchu, La La La dance video kutoka kwao Kings Music pamoja na video ya Pekecha kutoka kwake Phina.