Home » Mke Wa Jua Cali Lilly Asigo Afichua Waliachana 2022 Kwa Miezi Kadhaa

Mke Wa Jua Cali Lilly Asigo Afichua Waliachana 2022 Kwa Miezi Kadhaa

Lilly Asigo, mke wa msanii maarufu wa Genge, Jua Cali, amefichua kuwa waliachana kwa miezi kadhaa mwaka jana.

 

Katika mahojiano na Lofti Matambo kwenye kipindi cha Gumzo la Sato, Lilly alisema wakiwa wanandoa maarufu, uhusiano wao sio siri bali wanaishi bila kusambaza kila kitu kwenye mitandao ya kijamii.

 

“Hamjui ya kwamba mimi na Jua Cali tulikuwa tumeachana for months. Hakuna mtu alijuwa. Kwanini? Tunaishi privately. We’re not a secret but we have a private life.Tulikosana, na si kitambo, ni mwaka jana. Lakini sikuenda nikaposti nikasema huyu naye akanikosea ama naye pia kusema bibi yangu nini nini. Sometimes take time. Naweza kuwa nimekukosea kwasababu mimi ni binadamu lakini tunaweza solve bila kucomment.”

 

Alikataa kueleza sababu iliyowafanya wawili hao kutengana kwa miezi kadhaa, akisema ni suala la faragha ambalo lilitatuliwa kwa faragha.

 

Mnamo mwaka wa 2019, Lilly Asigo alifunguka jinsi alivyokaribia kuondoka nyumbani kwao.
Alifichua kuwa alikuwa na changamoto za kuzoea kuishi na rapper huyo kati ya mambo mengine.
Ufichuzi wake ulikuwa katika kujibu Juacali akisema kwamba anamheshimu sana kwa kujitolea kwake kwa ajili ya kazi yake.

 

Kutokana na uzoefu wake, Lilly alizidi kufichua kwamba kinachofanya ndoa iendelee ni yale ambayo wanandoa hufanya nyuma ya pazia.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!