Home » Nairobi Expressway Yatangaza Nafasi 50 Za Kazi, Hakuna Digrii Inayohitajika

Nairobi Expressway Yatangaza Nafasi 50 Za Kazi, Hakuna Digrii Inayohitajika

Kampuni ya Moja Expressway, inayosimamia Barabara ya Nairobi Expressway, imetangaza nafasi 50 za kazi kwa wakenya wote bila masharti ya kuwa digrii.

Katika notisi iliyochapishwa kwenye tovuti yake leo hii Jumatano, Machi 1, kampuni hiyo imetangaza kazi za kitengo cha mauzo ili kusukuma moja ya bidhaa inazotoa.

 

Kulingana na usimamizi, lengo la kuajiri wawakilishi wa mauzo ni kwa ajili ya Huduma ya Ukusanyaji Ushuru wa Kielektroniki (ETC) katika Barabara ya Nairobi Expressway.

 

Wakenya wanaovutiwa na nafasi hizo za ajira wameombwa kuwasilisha maombi yao ifikapo Machi 10.

 

Wawakilishi wa mauzo walipwa kwa kutangaza huduma ya ETC na kusajili watu watakaojiunga wapya kulingana na hitaji lao la kila mwezi.

 

Kwa kuongezea, watalazimika kujibu maswali kutoka kwa madereva wanaotumia barabara iliyoinuliwa na majukumu mengine yoyote kama watakavyoagizwa na msimamizi.

 

Waombaji lazima pia wakidhi ustadi na kizingiti cha uzoefu cha kufanya mauzo kwa angalau mwaka mmoja vile vile mtu awe ujuzi wa hali ya juu katika mauzo.

 

Aidha wanaovutiwa Wanapaswa pia kuonyesha ustadi wa huduma kwa wateja, uvumilivu na uamuzi, ustadi bora wa mawasiliano.

 

Kifaa cha ETC ni miongoni mwa chaguo ya malipo inayopatikana kwa madereva wanaotumia barabara hiyo ya mwendokasi.

 

Kifaa hicho huwekwa kwenye vioo vya mbele vya magari ili kuwaruhusu kulipa ada za ushuru bila kuingiliana na wafanyikazi katika vituo vya kutoza.

 

Jinsi ya kuomba mkenya anafaa kungia kwenye tovuti ya Kampuni ya Moja Expressway nairobiexpressway.ke.

 

Kwenye menyu ya juu, bofya chaguo la ‘Kazi’ ambalo hukuongoza kwenye ukurasa wa kazi.

 

Ukurasa ulio na fomu ya mtandaoni unaonekana. Jaza fomu hatua kwa hatua kupitia hatua saba kisha ubofye ‘Tuma Sasa’.

Taarifa zinazohitajika ni pamoja na maelezo ya kibinafsi, elimu, historia ya ajira, vyeti na leseni, ufumbuzi na sahihi ya kielektroniki.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!