Home » Wakenya Chini Ya shinikizo Zaidi Huku Mfumuko Wa Bei Ukipanda

Kuongezeka kwa bei za vyakula kumeendelea kuweka wakenya chini ya shinikizo na kuongeza gharama ya maisha, huku takwimu mpya zikionyesha kuwa mfumuko wa bei ulipanda hadi asilimia 9.2 mwezi Februari na baadhi ya gharama za vyakula zikipanda hadi asilimia 11 zaidi ya ilivyokuwa mwezi Januari.

 

Jana ripoti ya Ofisi ya Kitaifa ya Takwimu (KNBS) ilionyesha kuwa katika mwezi huo, bidhaa za chakula zilichangia pakubwa mfumuko wa bei, jambo linaloashiria maumivu ambayo Wakenya wanapitia kila siku.

 

Bei ya nyanya iliongezeka kwa asilimia 7.8 ikilinganishwa na Januari huku bei ya maziwa ambayo haijapakiwa ikiongezeka kwa asilimia 2.
Wakenya wameelezea mzigo mzito katka baadhi ya bidhaa za msingi kama vile kujaza gesi ya kupikia, ambayo bei yake iliongezeka kwa asilimia 4.7 mwezi Februari ikilinganishwa na Januari, hata bei ya umeme iliposhuka kwa kati ya asilimia 2.9 na 3.7.

 

KNBS pia imeripoti kuwa bei ya ngano na unga wa mahindi imeshuka kwa asilimia 2.4 na asilimia 2.5, mtawalia, katika mwezi huo, huku bei ya sukari ikishuka kwa asilimia 3.2.

 

Kiwango cha mfumuko wa bei cha asilimia 9.2 kinakuwa kiwango cha tatu cha juu zaidi kurekodiwa tangu mwaka jana, wakati Wakenya walipoanza kuhisi joto la bei ya juu ya bidhaa.

 

Mfumuko wa bei ulikuwa umepungua kutoka asilimia 9.1 mwezi Desemba hadi asilimia 9 mwezi Januari, baada ya kupanda kwa asilimia 9.5 mwezi Novemba na asilimia 9.6 mwezi Oktobakiwango cha juu zaidi katika zaidi ya miaka mitano.

 

Hata hivyo Kiwango cha mfumuko wa bei kilipanda zaidi ya kiwango cha juu cha Benki Kuu ya Kenya (CBK) kilichoongozwa na asilimia 7.5 katikati ya 2022 na kimebakia juu, na kusababisha hatua ya CBK kuongeza viwango vya mikopo kama hatua ya kudhibiti.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!