Home » PSC Yatangaza Nafasi Za Makamu Chansela Katika Vyuo Vikuu 10 Kote Nchini

PSC Yatangaza Nafasi Za Makamu Chansela Katika Vyuo Vikuu 10 Kote Nchini

Tume ya Utumishi wa Umma (PSC) imekaribisha maombi kutoka kwa watu waliohitimu na wanaovutiwa na nyadhifa za Makamu wa Chansela (VC) na naibu chansela (DVC) katika vyuo vikuu 10 kote nchini.

 

Katika tangazo Mkurugenzi mkuu wa PSC Simon Rotich amesema kuwa maombi hayo yanafaa kuwasilishwa kabla ya Machi 20 saa 17:00 jioni.

 

Vyuo vikuu vinavyotafuta nafasi ya VC ni Pwani, Kisii, Karatina, Chuo Kikuu cha Eldoret, Machakos, Chuo Kikuu cha Kusini Mashariki mwa Kenya, Chuo Kikuu cha Ufundi cha Kenya (TUK), Chuo Kikuu cha Kabianga, na Chuo Kikuu cha Alupe.

 

Watakaofaulu watapata marupurupu ya mshahara wa kila mwezi wa Ksh.474, 919  hadi Ksh.617,394 (Pwani, Kisii, Karatina, Kusini Mashariki mwa Kenya, Kabianga), Ksh.474,919 – Ksh.744, 078 (Eldoret, Alupe ), Ksh. 427,427 – Ksh.744,078 (Machakos), Ksh.425, 427– Ksh.744,078 (TUK).

 

Wakenya waliotimu wote wanatakiwa kuwa na PHD kutoka chuo kikuu kinachofahamika, wawe angalau na miaka 10 ya uzoefu wa kitaaluma na utafiti katika ngazi za juu, na wametumikia kwa kiasi kikubwa na matokeo yanayoonekana katika nafasi ya Mkuu wa Chuo Kikuu au kama Naibu Makamu wa Chansela wa chuo kikuu.

 

Nafasi ya manaibu chensela pia iko wazi katika vyuo vikuu vyote vilivyotajwa ikiwa ni pamoja na Chuo Kikuu cha Tom Mboya, mbali na TUK.
Kiwango cha malipo kwa watu binafsi katika kiwango hicho ni kati Ksh.427,427 hadi Ksh.547,106 pamoja na manufaa mengine.

 

Waombaji wanatakiwa kuwa angalau profesa mshiriki na aliyepata Ph.D. kutoka chuo kikuu kinachofahamika nchini Kenya, wana angalau miaka 8 ya uzoefu wa kitaaluma na utafiti katika nafasi ya mhadhiri mkuu, na angalau miaka 6 ya uzoefu wa maendeleo katika nafasi ya juu ya uongozi wa chuo kikuu kama vile mkuu, naibu mkuu wa chuo, au naibu makamu wa chansela.

 

Wagombea watahitajika kuwasilisha maombi yao kwa njia rasmi au kielektroniki.

 

Mkurugenzi Mtendaji Rotich amebainisha kuwa maombi yote yanapaswa kuwasilishwa pamoja na wasifukazi, nakala za kitambulisho au pasipoti, nakala za cheti cha kitaaluma, au hati nyingine zozote zinazohusika.
Wagombea walioorodheshwa watachapishwa kwenye wavuti ya tume.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!