Ofisi Ya Mdhibiti Wa Bajeti Inawahadaa Wakenya Kuhusu Matumizi Ya Kaunti, Adai Lusaka

Gavana wa Bungoma Kenneth Lusaka ameikashifu Ofisi ya Mdhibiti wa Bajeti akisema madai yake kuwa magavana wa kaunti wanatumia vibaya pesa za umma ni ya kupotosha.
Huku akihimiza mdhibiti wa bajeti kukomeshe kutoa habari za kupotosha, Gavana Lusaka amesema Baraza la Magavana litashughulikia suala hilo katika ngazi ya kitaifa.
Kuhusu kaunti yake, ameeleza kuwa matumizi ya kawaida ndio yamechangia kaunti hiyo kuitisha kiwango cha fedha kilichoagizwa cha milioni 150
Lusaka amesema ofisi ya bajeti pia inawahadaa watu kwa madai kwamba aliambulia patupu mara tu alipoapishwa kama mkuu wa kaunti.
Alizungumza katika viwanja vya Bumula wakati wa uzinduzi wa mradi wa bure wa mbolea, ambapo alitoa mbegu za mahindi na mbolea bila malipo kwa wakulima 21,900 walio katika mazingira magumu.
Baadhi ya wakulima 500 kutoka kwa kila kata 45 katika kaunti hiyo walinufaika.