Home » Madai Yaibuliwa Kuhusu Uuzaji Wa Nyama Ambayo Haijakaguliwa Katika Bucha Za Embu

Madai Yaibuliwa Kuhusu Uuzaji Wa Nyama Ambayo Haijakaguliwa Katika Bucha Za Embu

Maafisa wa afya ya umma kaunti ya Embu wameibua wasiwasi kuhusu kukithiri kwa uuzaji wa nyama ambayo haijakaguliwa ambayo imekumba miji mbalimbali ya kaunti hiyo.

 

Maafisa hao wamelezea wasiwasi wao baada ya zaidi ya kilo 300 za nyama ambayo haijakaguliwa kukamatwa kwenye usafiri wa barabarani katika mji wa Runyenjes huko Embu Mashariki.

 

Afisa Mkuu wa Afya ya Umma Daniel Mbogo amewaonya wamiliki wa bucha dhidi ya kuuza nyama ambayo haijakaguliwa.

 

Amesema walikamata zaidi ya mbuzi na kondoo 250 wiki iliyopita, ambao hawakukaguliwa na kuuzwa katika bucha za kienyeji.

 

Mbogo amesema maafisa wa afya ya umma wakipokea taarifa kutoka kwa wananchi waliwavamia baadhi ya watu waliokuwa wakivusha mizoga ya mbuzi wanne wakiwa tayari baadhi ya nyama zimeshagawiwa kwa wananchi.

 

Mbogo pia amehoji chanzo cha nyama kuonyeshwa kwenye bucha mbalimbali mjini Embu wakati vichinjio vimekuwa kusajili wastani wa ng’ombe watano hadi sita wanaochinjwa kila siku.

 

Aidha, amedai uchunguzi umeanzishwa na kuwataka maafisa wote wa umma kuhakikisha kuwa nyama zote zinazouzwa kwa wananchi zinakaguliwa na kugongwa mihuri na kutoa taarifa za ubadhilifu wowote utakaobainika ili kuwezesha kuchukuliwa hatua za haraka.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!