Home » Rais Ruto Ateua Jopo La Kuwaajiri Mwenyekiti Na Makamishna Wapya Wa IEBC.

Rais Ruto Ateua Jopo La Kuwaajiri Mwenyekiti Na Makamishna Wapya Wa IEBC.

President Ruto Lead In Mourning Londiani Junction Accident Victims

President William Ruto

Rais William Ruto amebuni jopokazi la uteuzi wa kuwaajiri waliopendekezwa kuteuliwa kuwa Mwenyekiti na wanachama wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC).

 

Kupitia Notisi ya Gazeti, Ruto ameteua jopo la wanachama saba, wiki mbili baada ya kutangaza nafasi zilizoachwa wazi katika baraza la uchaguzi, na hivyo kuandaa njia ya kuajiri makamishna wapya.

 

Rais ruto amewachagua Bethuel Sugut, Novince Euralia Atieno, Charity S. Kisotu, Evans Misati James, Benson Ngugi Njeri, Nelson Makanda na Fatuma Saman kuongoza zoezi hilo.

 

Mwezi uliopita, mkuu wa nchi alitia saini mswada wa marekebisho ya IEBC wa 2022 kuwa sheria unaoweka mazingira ya kuundwa kwa jopo la uteuzi la wanachama saba ili kuwaajiri makamishna wapya.

 

Jopokazi hilo sasa lilihitajika kuwa na wawakilishi wa Tume ya Huduma za Bunge, Tume ya Utumishi wa Umma (PSC), Kamati ya Uhusiano ya Vyama vya Kisiasa (PPLC), Chama cha Wanasheria wa Kenya (LSK), na Baraza la Dini Mbalimbali la Kenya.

 

Uteuzi huo unajiri saa chache baada ya jopo liloundwa kuchunguza ombi la kuondolewa afisini kwa Juliana Cherera, Francis Wanderi, Irene Masit na Justus Nyang’aya huku wajumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) wakiwasilisha ripoti yake kwa rais kukamilisha uamuzi wake.

 

Jopo hilo lilioongozwa na Jaji Aggrey Mucheule lilibainisha kuwa wasiwasi wa ukiukaji mkubwa wa Katiba wakati wa uchaguzi dhidi ya makamishna wanne umethibitishwa.

 

Cherera – aliyekuwa Makamu mwenyekiti wa IEBC – pamoja na Wanderi, Masit na Nyang’aya walipinga matokeo ya uchaguzi wa urais yaliyotangazwa na Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati mnamo Agosti 15, wakitaja “kutoweka” kwa jinsi yalivyofikiwa.

 

Baada ya Mahakama ya Juu kuidhinisha uchaguzi huo, maombi yaliwasilishwa kupinga kufaa kwao kushikilia wadhifa huo.

 

Kulingana na jopo linaloongozwa na Muchelule, Masit ambaye amesimamishwa kazi katika tume hiyo hadi kuamuliwa kwa maombi hayo, alikubali pendekezo la maajenti wa muungano wa Raila Odinga wa Azimio la Umoja-One la Kenya kusimamia matokeo ya uchaguzi wa urais na kulazimisha kurudiwa. .

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!