Home » Tetesi Za Uhusiano Kati Ya Nina Roz Na Sheebah Karungi Uganda Zanyooshwa

Nyota wa mziki kutoka nchini Uganda Nina Roz ameelezea kuhusu tetesi za kushiriki mapenzi ya jinsia moja na msanii mwenzake Sheebah Karungi.

 

Kwenye mahojiano yake hivi karibuni, mrembo huyo amesema taarifa za yeye kutoka kimapenzi na Sheebah hazina ukweli wowote bali yaliibuliwa na watesi wake waliokuwa na nia ya kumshusha kisanaa.

 

Aidha, amedai kuwa ukaribu wake na Sheebah ulikuwa wa kikazi ikizingatiwa kuwa alikuwa moja kati ya watu waliomshawishia kuasi maisha ya ufuska na kugeukia muziki.

 

Ikumbukwe kwamba Urafiki wa Nina Roz na Sheebah Karungi ulianza mwaka 2015 kwenye moja ya party iliondaliwa na meneja wa msanii Coco finger aitwaye Roland tangu kipindi hiko walikuwa wakijiachia sana kwenye viwanja mbali mbali vya kukulia bata kiasi cha watu kuanza kuhisi kuwa huenda wawili hao wanashiriki mapenzi ya jinsia moja kutokana na namna walivyokuwa wanaonesha mahaba mazito.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!