Jill Biden Asema Pembe Ya Afrika Inahitaji Misaada Zaidi Za Ukame
Mke wa Rais wa Marekani Jill Biden Jumapili, alitembelea jamii zilizoathiriwa na ukame nchini Kenya na kutoa wito kwa mataifa tajiri kutoa zaidi huku Pembe ya Afrika ikikabiliwa na hali mbaya zaidi katika miongo kadhaa.
Biden alihitimisha ziara yake ya mataifa mawili barani Afrika, kwa kutoa wito wa kuangaziwa zaidi juu ya ukame uliovunja rekodi ambao unatishia watu milioni 22 nchini Kenya, Somalia na Ethiopia na njaa.
Marekani imeweka sehemu kubwa ya bajeti ya msaada kwa ajili ya maafa ambayo yameua mamilioni ya mifugo na kuharibu mazao.
Biden alisikia maoni kutoka kwa wazazi wanaotatizika kulisha watoto wao na jamii ambazo haziwezi kupata maji ya kutosha baada ya misimu mitano ya mvua kushindwa.
Ukame ulikuwa lengo kuu la ziara ya Biden nchini Kenya, na mazungumzo mengine yakiangalia usalama wa chakula na kilimo katika hali ya hewa inayobadilika.
Lakini profesa wa chuo cha jumuiya mwenye umri wa miaka 71 pia alikutana na viongozi wa wanawake na vijana, akazuru makazi yasiyo rasmi, na kuweka shada la maua kwa wale waliouawa katika shambulio la bomu la ubalozi wa Marekani mjini Nairobi mwaka 1998.
Ziara yake nchini Kenya na kabla ya hapo Namibia inalenga kuendeleza Mkutano wa Viongozi wa Marekani na Afrika huko Washington mwishoni mwa mwaka jana ambapo Rais Joe Biden alisema nchi yake “imeingia” katika bara hilo lenye joto kali.
Afrika imekuwa uwanja mpya wa vita vya kidiplomasia kufuatia uvamizi wa Urusi nchini Ukraine mwaka jana na ziara ya Jill Biden ilikuwa ya kwanza kufanywa na afisa mkuu wa Ikulu ya Marekani barani humo tangu mumewe aingie madarakani.
Nchini Namibia, Biden alisema Marekani imejitolea kusaidia mataifa ya Afrika kupata sauti kubwa katika Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya kimataifa.