Home » Mtu Mmoja Afariki Na Wengine 42 Kujeruhiwa Baada Ya Ajali Naivasha

Mtu Mmoja Afariki Na Wengine 42 Kujeruhiwa Baada Ya Ajali Naivasha

Mtu mmoja amefariki na wengine 42 kujeruhiwa vibaya baada ya basi lililokuwa likielekea Nakuru kupata ajali eneo la Karai kwenye barabara kuu ya Naivasha-Nairobi jana Jumapili usiku.

 

Kamanda wa polisi wa Naivasha Samuel Waweru amesema majeruhi walikimbizwa katika hospitali ya kaunti ndogo ya Naivasha kwa matibabu.

 

Kulingana na Waweru, marehemu alifariki alipokuwa akisubiri kuhudumiwa katika Hospitali ya Kaunti Ndogo ya Naivasha.

 

Wasaidizi wa kwanza kutoka Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya na polisi walisaidia kuwapeleka majeruhi katika kituo cha afya.

 

Itakumbukwa kwamba Eneo ambalo ajali hiyo ilitokea ilitiwa doa jeusi kuashiria kuwa ajali nyingi zimekuwa zikitokea eneo hilo.

 

Mnamo mwaka wa 2017, zaidi ya watu 40 walifariki wakati moto kutoka kwa gari la mafuta kuwaka na kushika magari kadhaa.

 

Dereva alishindwa kulidhibiti lori hilo na kugongana na magari mengine, na kusababisha takriban watu 39, wakiwemo maafisa 11 wa kikosi cha Recce Kikosi cha General Service Unit, kuteketezwa ndani ya magari yao.

 

Maeneo mengine ambayo yametiwa alama hiyo ya ajali katika barabara kuu ya Nairobi-Nakuru ni pamoja na, Kinungi, Mbaruk, Gilgil na eneo la St Mary’s.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!