Home » Azimio kufanya mkutano wa kumpinga Ruto huko Jevanjee

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga leo asubuhi ataongoza wafuasi wake kwa mkutano wa kumpinga rais William Ruto katika bustani ya Jeevanjee jijini Nairobi.

 

Ikumbukwe Raila jana alisema manaibu wake wataendelea kushinikiza mageuzi ya uchaguzi, umoja wa nchi na kupunguza gharama ya juu ya maisha ambayo alisema inasumbua raia wa kawaida.

 

Akizungumza wakati wa mazishi ya kakake Prof Makau Mutua, Gabriel Wambua Mutua, Kitui jana, Raila alisema ingawa utawala wa Ruto uliahidi kupunguza gharama ya maisha, umekuwa ukiongeza ushuru, na hivyo kufanya maisha kuwa magumu.

 

Raila aliendelea kusisitiza kuwa ingawa baadhi ya Wakenya wamekuwa wakihoji ni kwa nini hawakupeleka masuala ya mtoa taarifa huyo katika Mahakama ya Juu, alisema maombi yao yalikataliwa.

 

Kulingana na Raila, haki ya kijamii na kiuchumi inaenda sambamba na harakati za kupigania haki katika uchaguzi na kuongeza kuwa tawala haramu hazijali wananchi bali zinajali takwimu tu, kiasi gani cha fedha kimekusanywa kwa ushuru, mkopo kiasi gani wa wananchi wamechukua; asilimia ambayo uchumi unakua.

Aidha Raila anasema utawala wa Ruto umekuwa na mwelekeo wa kuwatoza Wakenya ushuru lakini ukifanya kidogo sana kupunguza mateso hayo, akiongeza kuwa kwa kila bili ya maji ya Sh100, Sh70 hutozwa ushuru.

 

Alisema wakati wa kampeni hizo, Azimio uliahidi kutoa elimu kwa wote kuanzia chekechekea hadi chuo kikuu na kuongeza kuwa wazazi wengi hawawezi tena kuwapeleka watoto shule kwa sababu ya ughali wa maisha.

 

Hata hivyo, aliahidi kuwa wataanzisha mpango wa Hifadhi ya Jamii ambapo kaya maskini zitapewa posho ya Sh6000 kila mwezi ili kuwanusuru na hali mbaya ya umaskini na njaa.

 

Raila amesema kuwa timu yake ya Azimio itazunguka nchi nzima na kufanya mikutano ya hadhara kuwahamasisha juu ya hitaji la kupunguza gharama kubwa ya maisha ambayo imekuwa ngumu kwa wengi.

 

Kadhalika Alitilia mkazo maoni ya Naibu Rais Rigathi Gachagua ambapo alilinganisha Kenya kama kampuni, akisema kwamba mawazo ya viongozi hao wawili wakuu ni kugawanya nchi na vifuko vya kikabila na kuwaacha Wakenya wengine nje ya serikali.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!