Home » Gladys Shollei: Wanaohisi uchaguzi Ulitatizwa Wanapaswa Kufuata Mkondo Kisheria

Gladys Shollei: Wanaohisi uchaguzi Ulitatizwa Wanapaswa Kufuata Mkondo Kisheria

Naibu Spika wa Bunge la Kitaifa Gladys Boss Shollei amewasuta viongozi wanaodai kuwa uchaguzi wa Agosti 2022 ulivurugwa kuacha kunyoshea kidole cha lawama serikali tawala ya kenya kwanza.

 

Akiongea kwenye kipindi cha runinga moja humu nchini leo Jumatatu, Shollei amedai kuwa viongozi wanaoegemea upande wa upinzani wanaikashifu Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kwa madai ya kusimamia matokeo ya uchaguzi wa urais ilhali wanafurahia nyadhifa walizoshikilia ambazo walichaguliwa kupitia tume iyo hiyo.

 

Shollei amesema ikiwa viongozi hao wanafikiri kwamba IEBC haikufanya uchaguzi wa haki wanapaswa pia kujiuzulu na kutetea kile wanachoamini na kuacha kuzungumza mara mbili.

 

Shollei, ambaye ni mwakilishi wa Uasin Gishu Woman, alikuwa akijibu madai ya Seneta Onyonka kwamba tume ya uchaguzi itahujumiwa kila mara ikiwa wajumbe wengi wa baraza hilo watachagua watu wanaowapendelea zaidi kwenye tume hiyo.

 

Onyonka pia alidai kuwa mwelekeo uo huo ndio ulisababisha mzozo unaodaiwa kuwa wa uchaguzi wa Agosti 2022 kati ya serikali na upinzani.

 

Ibara ya 250 ya Katiba inasema kwamba mwenyekiti na kila mjumbe wa tume atatambuliwa na kupendekezwa kuteuliwa kwa utaratibu uliowekwa na sheria ya kitaifa, iliyoidhinishwa na Bunge na kuteuliwa na Rais.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!