Home » Ripoti Yafichua Wafanyikazi Hewa 1,300 Kaunti ya Kisii

Ripoti Yafichua Wafanyikazi Hewa 1,300 Kaunti ya Kisii

Siku moja baada ya kutolewa kwa Ripoti ya Ukaguzi wa Wafanyikazi wa Kaunti ya Kisii na Taasisi ya Usimamizi wa Rasilimali Watu, Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC), inasema pesa za umma zilizopotea Kisii lazima zirejeshwe.

 

Katika taarifa iliyotolewa na shirika la kupambana na ufisadi, EACC limesema litaanzisha kesi ya kurejesha mishahara yoyote iliyopatikana kwa msingi wa vyeti ghushi vya masomo ikisema ni sawa na kupatikana kwa mali ya umma kwa njia ya udanganyifu.

 

EACC pia imedokeza kuwa ripoti hiyo inajiri huku wakikamilisha uchunguzi dhidi ya wafisadi katika kaunti hiyo ambao wanadaiwa kunyonya hazina ya kaunti kupitia shughuli zao za ufisadi.

 

Kulingana na EACC, kaunti kadhaa nchini ziko kwenye rada zao kuhusiana na ripoti za ubadhirifu mkubwa wa pesa.

 

Taasisi ya Usimamizi wa Rasilimali za Kibinadamu (IHRM) ilitoa ripoti yake kwa Gavana wa Kaunti ya Kisii Simba Arati Jumatano baada ya miezi miwili ya ukaguzi wa kina wa wafanyikazi wa kaunti hiyo.

 

Katika ripoti hiyo, dosari kubwa zilibainishwa miongoni mwao kugunduliwa kwa wafanyakazi hewa 1,314, Ksh 48.7 milioni kama pesa iliyolipwa kupitia posho zisizo za kawaida, hati ghushi za masomo huku wengine pia wakiripotiwa kusitisha kama Watu Wenye Ulemavuna vyeti vya kughushi miongoni mwao.

 

Ripoti hiyo sasa inasubiri kuwasilishwa mbele ya baraza la mawaziri la Kaunti hiyo kwa hatua zaidi.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!